Nyumba ya Tembo yatima

Kila muhula, "Theologische Stifft" inasaidia mradi wa hisani kwa kuutangaza na kukusanya michango.

Katika muhula huu, tumevutiwa na Nyumba ya Tembo yatima nchini Kenya-Nairobi.Mradi unasaidia utunzwaji wa wanyama na viumbe hai na kuimarisha miundo mbinu ya kijamii.

Japokuwa ujangili wa pembe za ndovu ni kinyume cha sheria katika nchi nyingi, bado Tembo wanaendelea kuuwawa.Watoto wa Tembo wanaachwa yatima-kama binadamu- wanavyotegemea Mama zao kuishi.
Ngozi zao ni sensitivu sana katika jua.Wapo katika hatari dhidi ya wanyama walao nyama na pia wanashida ya kupata maji na kutumia mikonge yao sawa sawa.Msaada unatolewa na David Sheldrick Wildlife Trust Orphans Project. Watoto wa Tembo wanahudumiwa kila moja 24/7 na wanalishwa kwa maziwa maalumu.

Tembo kama wanyama wakijamii, wanajichagulia marafi wao wakiwa katika kitua cha Tembo yatima na baadae hujumuishwa katika maisha ya asilia katika mbuga ya Tsavo.Baadhi ya Tembo wenye umri mkubwa wamekuwa na desturi ya kuwachukua Tembo wadogo kutoka katika Kituo cha Tembo yatima na kuwafundisha maisha "Katika dunia asilia".
Miaka michache iliopita ilikuwa ni nyumba ya Tembo wachanga/wadogo, Wildlife Trust wametanua wigo wa kazi zao katika kuwakomboa na kuwajumuisha wanyama wengine kama Vifaru.
Cha kuvutia sana ni urafiki wa kudumu kati yao na baadhi ya Tembo.

Mradi huu ulianzishwa miaka ya 80 na Daphne Sheldrick, na kutunukiwa heshima na Malikia wakati akihudumia mradi wa yatima. Kwa Ujerumani, msaada unatoka katika jumuia iitwayo Rettet die Elefanten Afrikas "Okoa Tembo wa Afrika"-moja katika shughuli zao muhimu ni kuandaa ufadhili/kufadhili na kuhudumia Tembo.

Kwa pamoja jumuiya ya Ujerumani na Kituo cha Tembo yatima wanajishughulisha katika kukuza ufahamu ulimwenguni juu ya hatima (na matumaini) ya Tembo yatima, na pia kuutahadharisha umma wa Wakenya juu ya hatari zinazo wakabili Tembo kwa sasa-Ujangili, na pia kutoweka kwa makazi kunakosababishwa na ongezeko la idadi ya watu na migogoro, ukataji miti na ukame. Kwa kuongezea, hatua za utunzaji (mfano. Tanzania, Malawi na Uganda) zinahimizwa. Kituo kimekuwa kivutio cha watalii wanao vutiwa katika swala hili, na pia kutoa ajira kwa wakazi wa eneo husika-na hata Majangili.Kwa pamoja, Wanyama na watu wanasaidiwa na mradi wa Tembo-yatima.

Tunatoa shukrani zetu kwa michango zaidi kwa mradi wetu!. Kwa habari zaidi, jisikie huru kuangalia tovuti ifwatayo:

http://www.sheldrickwildlifetrust.org/


Karoline Pohl, Translator/Mtafsiri: Benson Elisamoni Matawana